Address
304 North Cardinal St.
Dorchester Center, MA 02124
Work Hours
Monday to Friday: 7AM - 7PM
Weekend: 10AM - 5PM
Address
304 North Cardinal St.
Dorchester Center, MA 02124
Work Hours
Monday to Friday: 7AM - 7PM
Weekend: 10AM - 5PM

Maarifa. Ubunifu na kasi

Karne na karne zimepita binadamu wamekuwa wakijishugulisha na biashara popote duniani. Tunashuhudia nchi na nchi au kampuni na kampuni kila kona ya dunia kila kunapokucha wanafunga mikataba ya kufanya biashara. Pia tunashuhudia katika dunia hii kasi ya kusafiri ya watu kutoka nchi moja kwenda nyingine au kutoka eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya biashara inaongezeka kila uchao. Ubunifu wa kila aina unafanyika ili kuhakikisha bidhaa zinauzika na zinapatikana kwa ubora wa hali ya juu kabisa. Kwa sababu hiyo ushindani wa kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu umeongezeka kwa kiwango kikubwa, maarifa yameongezeka kwenye kila eneo. Kuna makampuni makubwa na madogo yanazidi kuundwa kila kona ya dunia kila siku kwa ajili ya kufanya biashara.
Biashara ndiyo njia pekee iliyothibitishwa tangu vizazi vingi vilivyopita inayoweza kuleta faida kubwa ya kiuchumi. Ukiwa na ng’ombe wengi, ukiwa na mashamba mengi, ukiwa na madini wengi na rasilimali nyingine nyingi hizo zote hazitakusaidia wala hazitakuwa na thamani pasipo biashara. Kwa hiyo tunapata kufahamu kwamba tumeumbwa ili tupate faida kiuchumi kwa njia ya biashara.
Mkulima analima mazao ili apate chakula lakini pia ili apate faida kwa njia ya biashara, Mfugaji anafuga mifugo yake ili apate chakula lakini pia ili apate faida kwa njia ya biashara. Na kila mtu kwa kadri ya uwezo wake anafanya kila namna ili aweze kupata faida kwa njia ya biashara.
AGIZO MAALUMU
Siku moja kabaila mmoja aliwaita vibarua wake akawagawia mafungu ya fedha kila mmoja wao fungu moja la fedha, Kisha akawaambia FANYENI BIASHARA HATA NITAKAPOKUJA (Luka 19:13). Hilo lilikuwa ni agizo sio kwao tu bali pia hata kwetu sisi tunaoishi sasa, lwamba imetupasa kufanya biashara hata atakapokuja Mwana wa Adamu ulimwenguni kwa mara ya pili.
Vitabu vyote vya dini vinakiri wazi kwamba kufanya biashara katika misingi ya haki ni njia halali ya kupata mapato. Ikiwa vitabu hivyo vinaturuhusu kufanya biashara, maana yake vinatuagiza kufanya biashara; tunatakiwa kufanya biashara katika misingi ya haki na ukweli. Kama wewe unamwamini Mungu unaweza kujifunza pia katika maandiko haya kuhusiana na agizo hili la kufanya biashara; Mathayo 13: 45, Mathayo 25: 16, Yakobo 4:13, Mwanzo 34:10, Mwanzo 42: 34, Nehemia 13:16, Isaya 23:18, Ezekieli 17:4, Ezekieli 27:12, Mithali 31:10-28 nk
Hata mfalme Sulemani aliweza kuupata utajiri wake kwa kufanya biashara, kwani aliajiri watu wengi waliokuwa wanafanya biashara yake. 1Wafalme 10:28, 2 Mambo ya Nyakati 9:14 Kwahiyo imetupasa kufanya biashara ili tupate faida na utajiri ulio halali kwa misingi ya haki na kweli.
UMESHAANZA KUFANYA BIASHARA?
Ikiwa tayari unafanya biashara nikupongeze sana, labda nikukumbushe tu kwamba jitahidi sana kuwa mbunifu ili uweze kushindana katika masoko ya bidhaa. Kitu kingine nikukumbushe ni kwamba biashara bila haki ni utapeli na dhuluma vitu ambavyo vitakukosesha thawabu kwa Mwenyezi Mungu. Biashara ni biashara tu hata kama niya kubahatisha, kinachotakiwa ni kwamba jifunze kuipenda na kuiendesha kwa ustadi mkubwa.
Ikiwa mpaka dakika hii hujaanza kufanya biashara yoyote, unayonafasi bado ya kuanza kufanya biashara yako mapema iwezekanavyo ili utengeneze faida na uongeze mapato yako. Najua utakuwa una maswali mengi sana ya kujiuliza, mfano; Nifanye biashara gani? Nitapata wapi mtaji? Nitatoa wapi bidhaa za kuuza? Nitatumia mfumo upi kufanya biashara ikizingatiwa kwamba mimi sina uzoefu wowote katika biashara? Nakadhalika nakadhalika. Ikiwa una maswali ya namna hiyo, usihofu, ndiyo maana sisi Fikia Upeo tumejipanga kukusaidia kuyajibu maswali hayo kwa ufasaha. Ambatana nasi utazidi kufahamu.
NJIA ZA KUFANYA BIASHARA
Kwenye somo la historia tulikuwa tunasoma kwamba watu wa kale walikuwa wanafanya biashara kwa kubadilishana bidhaa kwa bidhaa. Mfano, walikuwa wanabadilishana dhahabu kwa shanga. Biashara hiyo iliitwa Barter System. Baadaye njia hiyo ya kufanya biashara ilipotea baada ya kugunduliwa kwa fedha. Kwahiyo mtu anabadilisha bidhaa au huduma kwa pesa. Njia zote hizi mbili yaani ile ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa na hii ya kubadilishana bidhaa kwa pesa, zinamlazimu mnunuzi au muuzaji kusafiri umbali mrefu ili kwenda kununua au kwenda kuuza bidhaa yake.
Njia mpya yagunduliwa.
Baada ya kugunduliwa kwa intaneti mfumo wa ufanyaji biashara umebadilika sana, sasa badala ya kutembea umbali mrefu kwenda kununua au kuuza bidhaa; unaweza kununua au kuuza bidhaa yoyote ile ukiwa chumbani kwako kwenye kompyuta yako. Hii inaitwa biashara kwa njia ya mtandao wa intaneti (e–commerce). Muuzaji huweka bidhaa yake au huduma yake kwenye mtandao wa intaneti kisha mnunuaji hununua bidhaa hiyo akiwa popote duniani bila kulazimika kuonana ana kwa ana na muuzaji. Tayari ufanyaji biashara kwa kutumia intaneti umekwisha kuenea popote duniani na ndiyo biashara inayoshika kasi katika karne hii ya 21.
Makampuni makubwa kama vile Amazon, Alibaba, Facebook, Whatsapp, Google, na mengine mengi yanafanya biashara kwa mfumo huu. Hapa kwetu Tanzania makampuni kadhaa tayari yanafanya biashara kwa mfumo huu.
Zaidi ya hayo, mamilioni ya watu kwa sasa ulimwenguni kote wanafanya biashara zao kwa kutumia mtandao wa intaneti. Wapo wanaouza vitabu, nyimbo na filamu (Audio na Video), program za kompyuta, wengine wanatoa mafunzo kwa njia ya intaneti na wengine wanauza kila aina ya bidhaa kama vile magari, pikipiki, vyakula, teknolojia nakadhalika.
Sisi hapa Fikia Upeo tumejikita kufundisha namna ya ufanyaji biashara kwa kutumia mtandao wa intaneti. Jinsi ya kutengeneza bidhaa za kiektroniki (e-goods), namna ya kutafuta wateja na namna ya kuongeza ubora wa bidhaa hizo ili uweze kushindana katika soko la bidhaa. Chukulia kwa mfano kampuni ya Amazon na Alibaba wanapata mamilioni ya dola kila siku kwa kufanya biashara kwa mfumo huu. Hata wewe chochote unachouza unaweza kukiweka kwenye mfumo huu kisha utapata wateja kutoka popote duniani. Haya ndiyo mageuzi tunayoyataka yatokee hapa Tanzania kwa kila mfanyabiashara ili aweze kuongeza kipato chake na kuinua uchumi wa mtu binafsi na taifa kwa ujumla.