Hobby yako

Hobby yako ni kazi unayoifanya mara baada ya kazi za kawaida za kila siku hasa muda wa mapumziko. Hobby yako inaweza kuwa ni kusoma vitabu, kuangalia mpira wa miguu, kutembelea maeneo yenye mandhari nzuri ya ufukweni, kufundisha, kucheza mpira na kadhalika. Hobby yoyote uliyonayo unaweza kuifanya kuwa biashara yako ukiamua. Kwa mfano kama wewe unapenda kuangalia mpira wa miguu, basi unaweza kufungua kibanda chako kisha ukakiandaa vizuri kabisa unanunua luninga yako kisha unaanza kuonyesha mpira. Badala ya wateja wako kulipa pesa ya kiingilio unaweka kiingilio ni kinywaji, hivyo mteja wako lazima anunue kinywaji ndipo aangalie mpira, nakwambia utapata wateja wengi.

Unaweza kuandaa blog au tovuti inayoelezea mambo ya kutembelea maeneo yenye mandhari nzuri kisha unawaalika watu kwenye tovuti hiyo kununua baadhi ya vitabu vyako vya maswala hayo au unaweza kuanzisha safari “Tour” ambapo watu wataungana na wewe kwenye “tour” hiyo. Kwahiyo kwenye kila hobby yako uliyonayo unaweza kuifanya kuwa biashara yako.

FOMU IFUATAYO ITAKUSAIDIA KUBAINI HUDUMA AU BIASHARA UNAYOWEZA KUIFANYA KWA KUTUMIA HOBBY YAKO

  1. Unapomaliza kufanya kazi zako za kila siku huwa unafanya nini hasa muda wa kupumzika?………………………
  2. Kwahiyo unafikiri hobby yako ni nini?………………….
  3. Kwa kutumia hobby yako hiyo, unaweza kufanya kitu gani kiwe kama huduma  kwa jamii?………………..
  4. Ukianzisha hiyo huduma utapata pesa kwa njia gani?………………….
  5. Vipi ushindani utaweza kupata wateja?……………………

Angalia mfano wa fomu iliyojazwa hapa chini

  1. Unapomaliza kufanya kazi zako za kila siku huwa unafanya nini hasa muda wa kupumzika?

Kuimba muziki

  • Kwahiyo unafikiri hobby yako ni nini?

Kuimba

  • Kwa kutumia hobby yako hiyo, unaweza kufanya kitu gani kiwe kama huduma  kwa jamii?

kutunga nyimbo za kuelimisha jamii

  • Ukianzisha hiyo huduma utaweza kupata pesa kwa njia gani?

Kuunza nyimbo hizo

  • Vipi ushindani utaweza kupata wateja?

Ndiyo, nitakuwa mbunifu sana, nitatunga wimbo wenye ujumbe mzuri na nitajitofautisha na waimbaji wengine. Ili kuhakikisha Napata wateja wengi nitaanzisha taasisi ya kufundisha au kuhamasisha vijana kuhusu uimbaji, zaidi ya yote nitaandika vitabu vinavyoelezea namna ya uimbaji. Kwa njia hiyo nitapata wateja wengi kwa sababu mpaka sasa hakuna mtu yeyote alieandika hata kitabu kimoja  kinachoelezea uimbaji.

Duniani kote maelfu ya watu mpaka dakika hii wanaingiza mamilioni ya dola kwa kutumia hobby zao. Ni wakati wa wewe kunufaika kwa kutumia hobby yako. Je uko tayari kunufaika kwa kutumia hobby yako?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *