Address
Fikia Upeo Co. Ltd
P.O.B ox 369 Bariadi-Simiyu-TZ
Phone: +255 785 661447

Maarifa. Ubunifu na kasi
KARIBU FIKIA UPEO
Kutafuta pesa na kutengeneza pesa yote ni mifumo ambayo inakuletea kipato. Mitego ya kutega pesa inaitwa vitega uchumi. Wahenga wanazo akili nyingi waligundua mapema wakakwepesha maneno, badala ya kusema vitega pesa wakasema vitega uchumi. Hata hivyo haileti maana kusema vitega uchumi kwa sababu neno uchumi ni pana mno sidhani kama unaweza kuutega uchumi, lakini pesa zinategeka. Mitego ya kutega pesa ni miradi ambayo inakuingizia kipato bila ya wewe kuhusika moja kwa moja katika nafasi ya ufanyakazi. Kumbuka sifa ya mitego mtegaji hutega kisha huondoka, atakuja baadaye kuona kama mtego wake umenasa pesa kisha huzichukua pesa japokuwa zina mabawa. Kitabu hiki kwa mapana na kwa mifano thabiti kimeandaliwa kukupitisha hatua kwa hatua katika eneo hili la kutega pesa kwa kutumia mitego ya kutega pesa iitwayo vitega uchumi

Tunawawezesha watu binafsi, wanafunzi, startups na wafanyabiashara kukuza uwezo wao kupitia elimu ya ujasiriamali, vitabu vya maendeleo binafsi na programu za ubunifu kwa watoto. Tunaamini kila mtu ana uwezo wa kufikia upeo wa ndoto zake
Tunatoa mafunzo na maarifa yanayowawezesha watu kuanzisha, kukuza na kusimamia biashara kwa mafanikio. Tunawasaidia wajasiriamali na biashara changa kupanga, kuendesha na kukuza shughuli zao kwa ufanisi.
Tunachapisha na kuuza vitabu vinavyotoa maarifa ya biashara, fedha binafsi, uwekezaji na maendeleo ya mtu binafsi.
Watoto Sing ni jukwaa linalotumia muziki, elimu na shughuli za vitendo kuwasaidia watoto kujifunza, kukuza vipaji na kujenga maadili mema. Kupitia nyimbo, matukio, bidhaa zenye chapa na shughuli mbalimbali, tunawajenga watoto kuwa viongozi wa kesho.
Tunatoa huduma za uchapishaji wa kalenda, vitabu, kadi za biashara, mabango, brosha na vifaa vya matangazo pamoja na branding ya kampuni.
Tunatengeneza maudhui ya kisasa ya kidijitali ikiwemo muziki wa AI, hadithi za watoto, video za elimu na miradi ya ubunifu.
Tunaisaidia biashara na taasisi kujenga uwepo wa kitaalamu mtandaoni kupitia tovuti, branding na suluhisho za kidijitali.

Kitabu
Siyo kupigana na mtu bali kupigana na umaskini, Lakini unafahamu jinsi ilivyo vigumu kupigana na adui usiyemwona kwa macho? Inahitaji maarifa na nidhamu ya kutosha vinginevyo haiwezekani kumshinda kabisa
Nimeandika kitabu hiki kwa sababu ya mwalimu anayenifundisha. Yupo mwalimu anayewafundisha watu wote kwa namna apendavyo yeye. Mwalimu huyu hutamkuta akiongea wala kuandika chochote wala hutasikia akipaaza sauti yake. Humfundisha kila mtu kwa njia ya matendo kwa jinsi apendavyo. Jina lake anaitwa MAISHA.
Kutokana na kasi kubwa ya mabadiliko, watu ambao wamekuwa hawabadiliki kulingana na ukuaji wa teknolojia wanajikuta wanashindwa kukua kiuchumi kwa sababu wanatumia njia zile zile za zamani ambazo zimepitwa wakati.

Watoto Sing ni kampuni ya ubunifu ya edutainment (elimu kupitia burudani) inayojikita katika kuwawezesha watoto kupitia muziki, usimulizi wa hadithi, ujifunzaji shirikishi, na shughuli mbalimbali za kimwili zinazovutia. Tunachanganya elimu na burudani ili kuwasaidia watoto kujifunza stadi muhimu za maisha, kujenga kujiamini, na kukua katika mazingira ya kufurahisha, salama, na yenye kuwahamasisha.
Ka Sungura: Wimbo unaopendwa zaidi na Watoto, unawafundisha ujasiri, ubunifu na kujiamini
Pori kwa Pori (Forest to Forest)- Watoto hujifunza utunza mazingira na vyanzo vya maji
Dr. Robot – Wimbo bora unaowahamasisha Watoto kuwa Madaktari, kutunza afya zao kwa kula vizuri na kufanya mazoezi
Kungfu Master- Watoto hawachoki kujifanya wao ni ma-kungfu Master baada ya kuutazama wimbo huu

Naomba nianze kwa kukuliza swali, ni jambo gani hujafanikiwa kulifanya kwa sababu ya kukosa utaalamu (maarifa)? Mfano linaweza kuwa ni biashara, kilimo, ufugaji, uendeshaji wa miradi, uongozi, uandishi, uwekezaji,au jambo jingine lolote. Kama kuna jambo la namna hiyo hujapata ufumbuzi wake na unakiu ya kulipatia ufumbuzi, makala hii inakuhusu wewe. Hakuna haja ya kubaki unahangaika…

Hobby yako ni kazi unayoifanya mara baada ya kazi za kawaida za kila siku hasa muda wa mapumziko. Hobby yako inaweza kuwa ni kusoma vitabu, kuangalia mpira wa miguu, kutembelea maeneo yenye mandhari nzuri ya ufukweni, kufundisha, kucheza mpira na kadhalika. Hobby yoyote uliyonayo unaweza kuifanya kuwa biashara yako ukiamua. Kwa mfano kama wewe unapenda…

Karne na karne zimepita binadamu wamekuwa wakijishugulisha na biashara popote duniani. Tunashuhudia nchi na nchi au kampuni na kampuni kila kona ya dunia kila kunapokucha wanafunga mikataba ya kufanya biashara. Pia tunashuhudia katika dunia hii kasi ya kusafiri ya watu kutoka nchi moja kwenda nyingine au kutoka eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya biashara…
Haya ni baadhi ya maoni chanya kutoka kwa wateja wetu

Asha Mwakalobo
Mjasiriamali
“Mafunzo ya Fikia Upeo yamebadilisha kabisa namna ninavyosimamia biashara yangu. Nilijifunza kutenganisha fedha za biashara na matumizi binafsi, jambo ambalo limeongeza faida na nidhamu ya kifedha.”

Abdul Hassan
Mjasiriamali
“Fikia Upeo wanatoa elimu ya fedha kwa lugha rahisi ambayo kila mtu anaweza kuelewa. Mafunzo yao yamenisaidia kufanya maamuzi bora ya kifedha na biashara.”

Esther Mushi
Mama wa Watoto
“Hizo nyimbo zenu za Watoto sing, watoto wangu hawabanduki kwenye TV, wanazipenda sana”