Watoto Sing ni brand ya watoto inayotumia muziki, ubunifu, elimu na burudani kuwasaidia watoto kujifunza maadili mema, kujiamini na kukuza vipaji vyao katika mazingira salama na yenye furaha. Mradi huu unasimamiwa na Fikia Upeo Company Limited.
Watoto Sing ni jukwaa la watoto linalounganisha muziki, elimu na ubunifu ili kuwajenga watoto wa kizazi cha sasa kuwa na maarifa, maadili na uwezo wa kujitambua.
Kupitia nyimbo za watoto, video za elimu, vitabu, michezo ya ubunifu na bidhaa mbalimbali za watoto, tunalenga kujenga mazingira ambayo mtoto anaweza kujifunza huku akifurahia utoto wake.
Tunataka watoto wa Afrika wakue wakijiamini, wakipenda kujifunza na kutumia vipaji vyao kuleta mabadiliko chanya duniani.
Dhamira Yetu
Kutoa elimu yenye ubunifu kwa watoto kupitia muziki, hadithi, video na bidhaa zinazowasaidia watoto kujifunza maadili mema, ubunifu, lugha, sayansi, utamaduni na maisha ya kila siku.
Maono Yetu
Kuwa brand kubwa ya watoto barani Afrika inayotumia muziki na burudani kuelimisha, kuhamasisha na kukuza vipaji vya watoto kwa viwango vya kimataifa.
Watoto Sing
Kwa Nini Uchague Watoto Sing?
#1 Elimu Yenye Furaha
Watoto hujifunza kupitia muziki na michezo kwa njia inayowavutia.
#2 Maadili Bora
Tunasisitiza heshima, upendo, uwajibikaji na nidhamu kwa watoto.
#3 Ubunifu wa Kisasa
Tunatumia teknolojia na ubunifu wa kisasa kutengeneza maudhui bora ya watoto.
#4 Utamaduni wa Kiafrika
Tunajivunia lugha, tamaduni na mazingira ya Kiafrika katika kazi zetu.
#5 Mazingira Salama kwa Watoto
Tunazingatia maudhui salama na yanayofaa kwa watoto wa rika zote.
#6 Kukuza Vipaji vya Watoto
Tunawawezesha watoto kugundua vipaji vyao katika kuimba, kucheza, kuigiza na ubunifu mwingine tangu wakiwa wadogo
HUDUMA ZIFUATAZO ZINAKUJIA HIVI KARIBUNI
T-shirt za Watoto zenye picha na majina ya nyimbo
Nguo nzuri zenye chapa nzuri kutoka Watoto Sing
Notebook, counter book na daftari kutoka Watoto sing
Tuungane Kujenga Kizazi Bora
Watoto wanahitaji elimu, ubunifu na mazingira mazuri ya kukuza ndoto zao. Kupitia Watoto Sing tunaamini mtoto anaweza kujifunza, kuimba, kucheza na kukua akiwa na furaha.
Jiunge nasi katika safari ya kuijenga brand kubwa ya watoto yenye maono ya kimataifa.